February 25, 2024

Simba yajihakikishia bilioni 2.5 za African Football League, bingwa kubeba bilioni 10

0
Spread the love

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika (“CAF”) limetangaza zawadi za mashindano ya Ligi ya Soka ya Afrika (“AFL”) yatakayoshirikisha vilabu vya soka vilivyo na viwango vya juu na vilivyo na mafanikio zaidi katika Bara la Afrika.

AFL itaanza Ijumaa tarehe 20 Oktoba 2023 jijini Dar es Salaam, Tanzani itawakilishwa na Simba SC itayofungua pazia la michuano hio dhidi ya Al Ahly SC ya Misri katika hatua ya robo fainali.

Vilabu vingine maarufu na vya juu zaidi vya kandanda vinavyoshiriki Uzinduzi wa AFL ni Enyimba FC (Nigeria), Wydad AC (Morocco), Mamelodi Sundowns FC (Afrika Kusini), TP Mazembe (DR Congo), Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) na Atlético Petróleos de Luanda (Angola).

Bingwa wa AFL anatarajiwa kubeba kitita cha Dola za Kimarekani Milioni 4 ambayo ni takribani Shilingi za Kitanzania Bilioni 10.

Timu zote nane zimejihakikishia kitita cha dola milioni moja sawa na takriban shilingi za Ktanzania bilioni mbili na nusu katika michuano hio itakayopigwa kwa mtindo wa mtoano wa mechi za nyumbani na ugenini.

AFL ni shindano la CAF lililoanzishwa kwa ushirikiano na FIFA. Mojawapo ya malengo makuu ya kuanzisha mashindano ya AFL ni kuhakikisha kwamba ubora wa kandanda ya Vilabu vya Afrika unashindana kimataifa na kwamba Vilabu vya Soka vya Afrika vinajiendesha kibiashara.

AFL pia itachangia katika kuibua na ukuzaji wa vipaji vya wanasoka Vijana katika Bara la Afrika. Nia ya CAF, ni kwamba Vyama vyote 54 Wanachama wa CAF ikiwa ni pamoja na nchi ambazo huenda hazina Vilabu vya soka katika AFL zifaidike na kupokea michango ya kifedha kutokana na uwezekano wa kupata mafanikio ya kibiashara kupitia AFL.

Pesa ya kwa washindi wa AFL ni kama ifuatavyo:

Bingwa : $4 000 000 kwa Mshindi
Mshindi wa Pili: $3 000 000
Kufuzu Nusu Fainali: $1 700 000
Robo Fainali: $1 000 000

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P