Simba yaburudika kileleni Ligi Kuu baada ya kuipiga Prisons 3-1

0

Mshambuliaji wa Simba John Bocco akishangilia bao lake dhidi ya Tanzania Prisons. (Picha:SSC_

Spread the love

Timu ya Simba imejitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Tanzania Prisons jioni ya leo katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Vijana wa kocha Robert Oliveira walilazimika kutoka nyuma kupata ushindi huo, kwani Edwin Balua alitangulia kuifungia dakika ya 12 baada ya kupiga mpira wa adhabu ulioenda moja kwa moja kwenye nyavu za kipa Ally Salum.

Saidi Ntibazonkiza akishangilia baada ya kufungwa mkwaju wa penati dhidi ya Tanzania Prisons. (SSC)

Clatous Chama aliisawazishia Simba dakika ya 34 akiunganisha krosi nzuri ya beki wa kulia Shomari Kapombe. John Bocco akaipeleka Simba mbele dakika za nyongeza kipindi cha kwanza kabla ya Said Ntibazonkiza kuihakikisha ushindi kwa kufunga mkwaju wa penati dakika ya 85.


Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi nne, ikifuatiwa na Azam pointi 10 mechi nne, Yanga pointi 9 mechi nne na Mashujaa wakiwa katika nafasi ya nne kwa pointi nane.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P