Sabato fundi wa vichwa, Prince Dube mapema zaidi

0
Spread the love

Mshambuliaji wa timu ya Polisi Tanzania, Kelvin Sabato, ameibuka kuwa kinara wa kufunga mabao mengi ya vichwa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23 iliyomalizika Juni 9.
Kwa mujibu wa takwimu za Ligi Kuu zilizotolewa baada ya ligi kumalizika, zinaonesha  Sabato ambaye timu yake imeshuka daraja, amefunga mabao matano kwa kutumia kichwa akiwa ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi ya aina hiyo msimu iliomalizika.


Takwimu zinaonyesha kuwa anafuatiwa na Mtanzania mwingine, Rafael Daudi wa Ihefu SC ambaye ametupia mara nne kwa kichwa.

Wachezaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jean Baleke na Henock Inonga wa Simba, pamoja na Fiston Mayele wa Yanga wote wanashika nafasi ya tatu kwenye ufungaji wa mabao ya vichwa, kila mmoja akipachika matatu.

Prince akishangalia mojawapo ya bao lake kati Ligi (Picha Hisani/Azam)


Wakati huo huo, bao la Prince Dube wa Azam FC alilolifunga sekunde ya 15 dhidi ya Simba limeweka rekodi ya kuwa bao la mapema zaidi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022/23.
Mzimbabwe huyo alifunga bao sekunde ya 15, katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Februari 21 mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Nickson Kibabage wa Mtibwa Sugar akifunga bao sekunde ya 28, timu yake ikicheza dhidi ya Mbeya City, Ismail Mgunda wa Prisons nafasi ya tatu kwa bao lake la dakika ya kwanza.
Henock Inonga na Moses Phiri wote wa Simba,  wanakamata nafasi ya nne kwa mabao yao ya dakika ya pili, Phiri akifunga dhidi ya KMC, Inonga akifunga dhidi ya Yanga, Aprili 16 mwaka huu, Uwanja wa Benjamin Mkapa, timu yake ikishinda mabao 2-0.

Ally Kipemba wa Polisi Tanzania alifunga dakika ya tatu dhidi ya KMC na Matheo Antony wa KMC alifunga katika dakika hiyo dhidi ya Ihefu SC, wakiwa kwenye nafasi ya tano.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P