Mfumo mpya wa Ligi Kuu Misri msimu ujao

0

Al Ahly

Spread the love

Mfumo mpya utatumika katika Ligi Kuu ya Misri kuanzia msimu ujao wa 2024/2025, rais wa Ligi y Misri, Ahmed Diab aamethibitisha.

Tangu kuzuka kwa janga la UVIKO-19 mnamo 2020, ligi ya Misri imekuwa na changamoto ya kumaliza msimu ndani ya muda maaalum na pia kuahirishwa kwa mechi mara kadhaa jambo linaloathiri vilabu kiuchumi.

Kulingana na Diab, mfumo wa Ligi ya Misri hautabadilishwa kwenda kwenye muundo wa makundi mawili kama ilivyopendekezwa awali bali utabadilika kuwa muundo mwingine kama Ligi ya Ubelgiji.

“Mashindano hayo yatagawanywa katika hatua mbili. Hatua ya kwanza itakuwa ya raundi moja na vilabu vilivyo katika nafasi za juu {katika nusu ya kwanza ya msimamo} vitafuzu kwa hatua inayofuata ili kuwania taji hilo kwa pointi zile zile walizokusanya hatua ya kwanza,” Diab alieleza.

“Vilabu vilivyosalia {katika nusu ya pili ya msimamo} vitachuana katika hatua ya pili pia wakiwa na pointi zilezile walizokusanya hatua ya kwanza ili kupata timu zinazoshuka daraja na pia viwango vingine vya msimamo,” aliongeza.

Diab alipongeza muundo huo mpya uliopendekezwa, akisisitiza kwamba itaokoa miezi miwili kutoka kwa ratiba ya kawaida kwani ligi itaanza katikati ya Septemba na kumalizika Mei.

Mnamo Jumatatu, Diab alisema kuwa msimu wa sasa wa 2023/24 utakamilika katikati ya Agosti, akipuuza ripoti zinazopendekeza mashindano ya ndani yangeendelea hadi Oktoba au Novemba.

Kwa sasa, Enppi inashikilia nafasi ya juu kwa muda kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 23 baada ya kucheza michezo 13 msimu huu.

Hata hivyo, mabingwa watetezi Ahly wanajikuta katika nafasi ya 9 wakiwa na pointi 17 katika michezo saba pekee kutokana na kushiriki katika michuano mbalimbali ya Kimataifa.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P