Gamondi ajitetea kupangua kikosi dhidi ya Ihefu

0
Spread the love

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ametetea uamuzi wake wa kupangua kikosi chake dhidi ya Ihefu siku ya Jumatano.

Mwanzo mzuri kabisa wa Young Africans katika Ligi Kuu ya NBC ulifikia kikomo walipopata kipigo chao cha kwanza kwenye msimu kufuatia kufungwa mabao 2-1 na Ihefu.

Wakiwa ugenini kwa mara ya kwanza msimu huu, Yanga walichukua uongozi mapema kipindi cha kwanza pale Pacome Zouzoua alipokamilisha kazi nzuri ya na Clement Mzize kuiandika bao la kwanza.

Young Africans walitawala sehemu kubwa ya umiliki wa mpira lakini wakawaruhusu Ihefu kusawazisha kwa mkwaju wa faulo dakika tano kabla ya mapumziko. Kipa Djigui Diarra aliutema mpira wa adhabu uliopigwa na Never Tigere na kumpa nafasi Lenny Kisu kuumalizia kwa kichwa.

Kipindi cha pili, shambulizi lingine la kasi lilishuhudia mpira ukitua miguuni mwa Charles Ilamfia ambaye alifunga bao la ushindi na kuifanya Yanga kudondosha pointi tatu.

“Nadhani bao la kwanza tulilofungwa tuliwapa zawadi. Tuliadhibiwa kwa makosa mawili tuliyofanya, tulijaribu kucheza nyuma kwa sababu tulisema uwanja sio mzuri hivyo tuwe na tahadhari. Kisha kipa akafanya makosa, hutokea kwenye soka japo ukweli ni kuwa ni kosa jepesi.”

“.Tulicheza vizuri sana kipindi cha kwanza na nadhani katika mechi tofauti tungeweza kwenda mapumziko tukiwa tunaongoza.”

“Katika bao la pili, walipafanya shambulizi la kushtukiza. Tulijua kwamba hatukuwa salama tulipokuwa tukishambulia. Kwa bao la pili wanakimbia mita 40. Tunaweza kujilaumu kwa hilo. Baada ya hapo nadhani hakukuwa na mpira tena kwa sababu mambo yaliyoendelea yalikuwa ni kinyume na soka.Kilichotokea baada ya hapo sio soka tena.”

“Simlaumu mwamuzi lakini hayuko katika kiwango cha kusimamia mchezo kama huo. Unaweza kuona mchezaji ambaye hataki kucheza, wanajiangusha na kupoteza muda. Lakini tumefungwa si kwa sababu ya mwamuzi bali kwa makosa yetu. Hatukuweka mpira wavuni.”

“Nimesikitishwa sana na matokeo lakini ni soka. Ni mechi nne pekee lakini tunatakiwa kufikiria kuhusu mechi inayofuata.”

“Mabadiliko yalikuwa sawa. Tulikuwa tunaongoza kabla ya kufanya makosa. Sio kwa sababu ya mabadiliko. Soka ni mchezo usio na haki, ningeshinda mchezo wangesema huyu ni kocha mkubwa kwa sababu ya mabadiliko. Na sasa kwa kuwa tumepoteza, huenda wakauliza kwa nini nilifanya mabadiliko. Hatuwezi kamwe kuwafurahisha watu 100%. Hata nilipofanya mabadiliko kipindi cha pili hatukupata tulichotarajia. Ni soka.”

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P