Cedric Kaze akiri kazi nzito Namungo

0

Kikosi cha Namungo

Spread the love

Namungo imeshindwa kufurukuta katika mechi mbili za mwanzoni mwa msimu huu, kocha mkuu wa kikosi hicho, Cedric Kaze akisema ana kazi ya kubadili uchezaji wa timu yake.

Kaze alisema kikosi chake kinaonesha mabadiliko, lakini nyota wake wanahitaji muda kuendana na kuweza kumudu kucheza soka la kisasa la kumiliki mpira na kushambulia ili kuachana na mfumo wa kupaki basi na kushambulia kwa kushtukiza waliouzoea.

Cedric Kaze (Picha: Namungo)

“Hatujaanza vizuri Ligi kwa ujumla lakini kutoka mchezo wa kwanza wa JKT Tanzania kuelekea mchezo wa pili wa KMC nimeona mabadiliko makubwa kubwa katika kumiliki mpira, kukaba tunapopoteza mpira na kutengeneza nafasi. Kwenye mchezo na KMC ni bahati mbaya hatukufunga lakini ukiangalia tathmini tumefanya mashuti yetu yaliyolenga lango ni karibu saba, pia karibu nafasi nne tuliweza kutengeneza za kukabiliana na kipa ana kwa ana.”

“Kitu kikubwa ni mchakato tulionao wa kujitahidi kubadilisha timu kutoka kukaa,kusubiri na kuzuia na kutegemea mashambulizi ya kushtukiza na mbio kwenda kwenye timu inayokamata na kutawala mchezo, inayoweza kumiliki mpira ikaenda mbele na kurudi nyuma. Ni mchakato mrefu.”

Namungo imeanza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kusuasua msimu huu. Wamecheza mechi mbila bila ya kupata ushindi licha ya kuwa mbele ya mashabiki wake katika uwanja wa Majaliwa. Ilianza kwa kufungwa bao 1-0 na JKT Tanzania na kisha kuambulia sare ya mabao 1-1 katika mchezo wa pili dhidi ya KMC.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P