February 25, 2024

Bakari Shime: Tuliwaheshimu Nigeria

0

Kikosi cha timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite kilichoanza katika sare ya kufungana bao 1-1 na Nigeria.

Spread the love

Kocha wa timu ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 20, (Tanzanite Queens) Bakari Shime amesema waliwapa heshimu kubwa wapinzani wao Nigeria katika mchezo wa kwa kwanza.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Chamazi Jumapili mchana, wenyeji, Tanzanite Queens walitoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao 1-1 dhidi ya taifa hilo lenye mafanikio makubwa zaidi katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA kwa Wanawake U-20.

Nigeria walipata bao la kuongoza dakika ya 57 kutokana na bao la mchezaji la Chioma Olise kufuatia kipindi cha kwanza kumalizika bila bao kwa pande zote.

Dakika 13 baadaye, Tanzanite Queens walijibu mapigo baada ya Asnath Ubamba kufunga kwa mpira wa adhabu na kumwacha kipa wa Nigeria, Anderlin Mgebchi akiwa hana la kufanya. Licha ya majaribio kadhaa kutoka kwa Tanzania, timu hiyo ya Afrika Magharibi ilifanikiwa kupata sare ya ugenini.

“Tuko katika uwanja wa nyumbani, tulitaraji tucheze vizuri na kupata ushindi. Kwa bahati mbaya hatukupata matokeo mazuri kwa maana ya kupata ushindi. Lakini tumetoka sare kwa maana ya sare ya mabao 1-1. Mechi bado iko wazi.”

“Vijana walicheza vizuri kufuata maelekezo. Tulicheza tukiamini tunacheza dhidi ya timu imara yenye uzoefu mkubwa, namna gani ya kushambulia na kujilinda. Kwa bahati mbaya tumefanya kosa la kushindwa kuokoa mpira ambao ulikuwa unazagaa eneo letu na wenzetu wakalitumia.”

“Mwisho wa siku tulijaribu kubadili plan ya kucheza. Tuliwasukuma kwenye eneo lao na tukapata free kick na kurudisha goli. Magoli ni 1-1, tunaamini mechi bado iko wazi. Tunaamini tumewaona kile ambacho wanacho na tunayo nafasi ya kufanya mabadiliko katika mechi inayofuata.”

“Tulikuwa hatuwafahamu lakini tuliwapa heshima kubwa sana kuhakikisha kwamba wasije kutuadhibu kwa matokeo ambaya zaidi tukiwa nyumbani kwetu. Tumeona aina yao y kucheza, hawatupi nafasi, wanafanya pressing za nguvu. Mwisho wa siku tunaamini na sisi tunaenda kucheza katika uwanja wao wa nyumbani na matokeo yakiwa wazi, goli 1-0 tunaweza kuwaondoa katika mashindano.”

“Tunaamini siku chache zilizobakia wasichana walikuwa na hofu ya kucheza na Nigeria tutawaondoa hofu. Hofu yao itaondoka na tunaamini tutakuwa free kucheza mpira wetu na kupata matokeo mazuri.”

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

P